Index   1  2  3  4  5  6  7  8  9  10  11  12  13  14  15  16  17  18  19  20  21  22  23  24  25  26  27  28  29  30  31  32  33  34  35  36  37  38  39  40  41  42  43  44  45  46  47  48  49  50  51  52  53  54  55  56  57  58  59  60  61  62  63  64  65  66  67  68  69  70  71  72  73  74  75  76  77  78  79  80  81  82  83  [84]  85  86  87  88  89  90  91  92  93  94  95  96  97  98  99  100  101  102  103  104  105  106  107  108  109  110  111  112  113  114 
AL INSYIQAAQ

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.

[84.1] Itapo chanika mbingu,

[84.2] Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,

[84.3] Na ardhi itakapo tanuliwa,

[84.4] Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu,

[84.5] Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza,

[84.6] Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta.

[84.7] Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia,

[84.8] Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi,

[84.9] Na arudi kwa ahali zake na furaha.

[84.10] Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake,

[84.11] Basi huyo ataomba kuteketea.

[84.12] Na ataingia Motoni.

[84.13] Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake.

[84.14] Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena.

[84.15] Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona!

[84.16] Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa,

[84.17] Na kwa usiku na unavyo vikusanya,

[84.18] Na kwa mwezi unapo pevuka,

[84.19] Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka!

[84.20] Basi wana nini hawaamini?

[84.21] Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu?

[84.22] Bali walio kufuru wanakanusha tu.

[84.23] Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria.

[84.24] Basi wabashirie adhabu chungu!

[84.25] Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika.